Zab. 69:2-10 Swahili Union Version (SUV)

2. Ninazama katika matope mengi,Pasipowezekana kusimama.Nimefika penye maji ya vilindi,Mkondo wa maji unanigharikisha.

3. Nimechoka kwa kulia kwangu,Koo yangu imekauka.Macho yangu yamedhoofuKwa kumngoja Mungu wangu.

4. Wanaonichukia bure ni wengiKuliko nywele za kichwa changu.Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari,Adui zangu kwa sababu isiyo kweli.Hata mimi nalilipishwa kwa nguvuVitu nisivyovichukua.

5. Ee Mungu, unajua upumbavu wangu,Wala hukufichwa dhambi yangu.

6. Wanaokungoja Wewe wasiaibishwe,Kwa ajili yangu, Bwana, MUNGU wa majeshi.Wanaokutafuta Wewe wasifedheheshwe,Kwa ajili yangu, Ee Mungu wa Israeli.

7. Maana kwa ajili yako nimestahimili laumu,Fedheha imenifunika uso wangu.

8. Nimekuwa mgeni kwa ndugu zangu,Na msikwao kwa wana wa mama yangu.

9. Maana wivu wa nyumba yako umenila,Na laumu zao wanaokulaumu zimenipata.

10. Nilipolia na kuiadhibu roho yangu kwa kufunga,Ikawa laumu juu yangu.

Zab. 69