1. Ee Mungu, uniokoe,Maana maji yamefika mpaka nafsini mwangu.
2. Ninazama katika matope mengi,Pasipowezekana kusimama.Nimefika penye maji ya vilindi,Mkondo wa maji unanigharikisha.
3. Nimechoka kwa kulia kwangu,Koo yangu imekauka.Macho yangu yamedhoofuKwa kumngoja Mungu wangu.
4. Wanaonichukia bure ni wengiKuliko nywele za kichwa changu.Watakao kunikatilia mbali wamekuwa hodari,Adui zangu kwa sababu isiyo kweli.Hata mimi nalilipishwa kwa nguvuVitu nisivyovichukua.
5. Ee Mungu, unajua upumbavu wangu,Wala hukufichwa dhambi yangu.