5. Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,Mungu katika kao lake takatifu.
6. Mungu huwakalisha wapweke nyumbani;Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa;Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu.
7. Ee Mungu, ulipotoka mbele ya watu wako,Ulipopita nyikani,
8. Nchi ilitetemekaNaam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu;Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.
9. Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema;Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.
10. Kabila yako ilifanya kao lake huko;Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa.
11. Bwana analitoa neno lake;Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;
12. Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia;Na mwanamke akaaye nyumbani agawa nyara.