26. Mhimidini Mungu katika mikutano,Bwana katika makusanyiko ya Israeli.
27. Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao;Wakuu wa Yuda, kundi lao;Wakuu wa Zabuloni;Wakuu wa Naftali.
28. Ee Mungu, uziamuru nguvu zako;Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu.
29. Kwa ajili ya hekalu lako YerusalemuWafalme watakuletea hedaya.
30. Mkemee mnyama wa manyasini;Kundi la mafahali, na ndama za watu;Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha,Uwatawanye watu wapendao vita.
31. Masheki watakuja kutoka Misri,Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara.
32. Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu,Msifuni Bwana kwa nyimbo.
33. Apandaye mbingu za mbingu za tangu milele;Aitoa sauti yake, sauti ya nguvu.
34. Mhesabieni Mungu nguvu;Enzi yake i juu ya Israeli;Na nguvu zake zi mawinguni.