Zab. 68:22-25 Swahili Union Version (SUV)

22. Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha,Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari;

23. Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako,Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake.

24. Ee Mungu, wameiona miendo yako;Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu

25. Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda,Kati ya wanawali wapiga matari.

Zab. 68