6. Aligeuza bahari ikawa nchi kavu;Katika mto walivuka kwa miguu;Huko ndiko mlikomfurahia.
7. Atawala kwa uweza wake milele;Macho yake yanaangalia mataifa;Waasio wasijitukuze nafsi zao.
8. Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu,Itangazeni sauti ya sifa zake;
9. Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai,Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe.
10. Kwa maana umetupima, Ee Mungu,Umetujaribu inavyojaribiwa fedha.
11. Ulituingiza ndani ya wavu,Na kuweka viunoni mwetu mzigo uliotulemea.