10. Kwa maana umetupima, Ee Mungu,Umetujaribu inavyojaribiwa fedha.
11. Ulituingiza ndani ya wavu,Na kuweka viunoni mwetu mzigo uliotulemea.
12. Uliwapandisha watuJuu ya vichwa vyetu.Tulipita motoni na majini;Ukatutoa na kutuleta kunako wingi.
13. Nitaingia nyumbani mwako na kafara;Nitaondoa kwako nadhiri zangu;
14. Ambazo midomo yangu ilizinena;Kinywa changu kikazisema nilipokuwa taabuni.
15. Kafara za vinono nitakutolea,Pamoja na fukizo la kondoo waume,Nitatoa ng’ombe pamoja na mbuzi.
16. Njoni, sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu,Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.