1. Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu;Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.
2. Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya,Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;
3. Waliounoa ulimi wao kama upanga,Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,
4. Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
5. Walijifanya hodari katika jambo baya;Hushauriana juu ya kutega mitego;Husema, Ni nani atakayeiona?