Zab. 58:7-10 Swahili Union Version (SUV)

7. Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi;Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.

8. Kama konokono ayeyukaye na kutoweka,Kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua,

9. Kabla ya masufuria yenu kupata moto wa miiba,Ataipeperusha kama chamchela,Iliyo mibichi na iliyo moto.

10. Mwenye haki atafurahi akionapo kisasi;Ataiosha miguu yake katika damu ya wasio haki.

Zab. 58