Zab. 58:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Ni kweli, enyi wakuu, mnanena haki?Enyi wanadamu, mnahukumu kwa adili?

2. Sivyo! Mioyoni mwenu mnatenda maovu;Katika nchi mnapima udhalimu wa mikono yenu.

3. Wasio haki wamejitenga tangu kuzaliwa kwao;Tangu tumboni wamepotea, wakisema uongo.

4. Sumu yao, mfano wake ni sumu ya nyoka;Mfano wao ni fira kiziwi azibaye sikio lake.

5. Asiyeisikiliza sauti ya waganga,Ijapo wanafanya uganga kwa ustadi.

6. Ee Mungu, uyavunje meno yao vinywani mwao;Ee BWANA, uyavunje magego ya wana-simba.

7. Na watoweke kama maji yapitayo kwa kasi;Akiielekeza mishale yake, iwe imetiwa ubutu.

8. Kama konokono ayeyukaye na kutoweka,Kama mimba iliyoharibika, isiyoliona jua,

Zab. 58