Zab. 57:7-10 Swahili Union Version (SUV)

7. Ee Mungu, moyo wangu u thabiti,Moyo wangu u thabiti.Nitaimba, nitaimba zaburi,

8. Amka, utukufu wangu.Amka, kinanda na kinubi,Nitaamka alfajiri.

9. Ee Bwana, nitakushukuru kati ya watu,Nitakuimbia zaburi kati ya mataifa.

10. Maana fadhili zako ni kubwa hata mbinguni,Na uaminifu wako hata mawinguni.

Zab. 57