11. Usinitenge na uso wako,Wala roho yako mtakatifu usiniondolee.
12. Unirudishie furaha ya wokovu wako;Unitegemeze kwa roho ya wepesi.
13. Nitawafundisha wakosaji njia zako,Na wenye dhambi watarejea kwako.
14. Ee MUNGU, Mungu wa wokovu wangu,Uniponye na damu za watu,Na ulimi wangu utaiimba haki yako.