1. Ee Mungu, unirehemu,Sawasawa na fadhili zako.Kiasi cha wingi wa rehema zako,Uyafute makosa yangu.
2. Unioshe kabisa na uovu wangu,Unitakase dhambi zangu.
3. Maana nimejua mimi makosa yanguNa dhambi yangu i mbele yangu daima.
4. Nimekutenda dhambi Wewe peke yako,Na kufanya maovu mbele za macho yako.Wewe ujulikane kuwa una haki unenapo,Na kuwa safi utoapo hukumu.
5. Tazama, mimi naliumbwa katika hali ya uovu;Mama yangu alinichukua mimba hatiani.
6. Tazama, wapendezwa na kweli iliyo moyoni;Nawe utanijulisha hekima kwa siri,
7. Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi,Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji
8. Unifanye kusikia furaha na shangwe,Mifupa uliyoiponda ifurahi.