Zab. 50:7-17 Swahili Union Version (SUV)

7. Sikieni, enyi watu wangu, nami nitanena,Mimi nitakushuhudia, Israeli;Mimi ndimi niliye MUNGU, Mungu wako.

8. Sitakukemea kwa ajili ya dhabihu zako,Na kafara zako ziko mbele zangu daima.

9. Sitatwaa ng’ombe katika nyumba yako,Wala beberu katika mazizi yako.

10. Maana kila hayawani ni wangu,Na makundi juu ya milima elfu.

11. Nawajua ndege wote wa milima,Na wanyama wote wa mashamba ni wangu

12. Kama ningekuwa na njaa singekuambia,Maana ulimwengu ni wangu, navyo viujazavyo.

13. Je! Nile nyama ya mafahali!Au ninywe damu ya mbuzi!

14. Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru;Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.

15. Ukaniite siku ya mateso;Nitakuokoa, na wewe utanitukuza.

16. Bali mtu asiye haki, Mungu amwambia,Una nini wewe kuitangaza sheria yangu,Na kuliweka agano langu kinywani mwako?

17. Maana wewe umechukia maonyo,Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.

Zab. 50