19. Umekiachia kinywa chako kinene mabaya,Na ulimi wako watunga hila.
20. Umekaa na kumsengenya ndugu yako,Na mwana wa mama yako umemsingizia.
21. Ndivyo ulivyofanya, nami nikanyamaza;Ukadhani ya kuwa Mimi ni kama wewe.Walakini nitakukemea;Nitayapanga hayo mbele ya macho yako.
22. Yafahamuni hayo,Ninyi mnaomsahau Mungu,Nisije nikawararueni,Asipatikane mwenye kuwaponya.