Zab. 50:17-20 Swahili Union Version (SUV)

17. Maana wewe umechukia maonyo,Na kuyatupa maneno yangu nyuma yako.

18. Ulipomwona mwivi ulikuwa radhi naye,Ukashirikiana na wazinzi.

19. Umekiachia kinywa chako kinene mabaya,Na ulimi wako watunga hila.

20. Umekaa na kumsengenya ndugu yako,Na mwana wa mama yako umemsingizia.

Zab. 50