Zab. 50:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Mungu, Mungu BWANA, amenena, ameiita nchi,Toka maawio ya jua hata machweo yake.

2. Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri,Mungu amemulika.

3. Mungu wetu atakuja wala hatanyamaza,Moto utakula mbele zake,na tufani yavuma sana ikimzunguka pande zote.

4. Ataziita mbingu zilizo juu,Na nchi pia awahukumu watu wake.

5. Nikusanyieni wacha Mungu wanguWaliofanya agano nami kwa dhabihu.

6. Na mbingu zitatangaza haki yake,Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu.

7. Sikieni, enyi watu wangu, nami nitanena,Mimi nitakushuhudia, Israeli;Mimi ndimi niliye MUNGU, Mungu wako.

Zab. 50