Zab. 5:1-5 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee BWANA, uyasikilize maneno yangu,Ukuangalie kutafakari kwangu.

2. Uisikie sauti ya kilio changu,Ee Mfalme wangu na Mungu wangu,Kwa maana Wewe ndiwe nikuombaye.

3. BWANA, asubuhi utaisikia sauti yangu,Asubuhi nitakupangia dua yangu na kutazamia.

4. Maana huwi Mungu apendezwaye na ubaya;Mtu mwovu hatakaa kwako;

5. Wajivunao hawatasimama mbele za macho yako;Unawachukia wote watendao ubatili.

Zab. 5