5. Kwa nini niogope siku za uovu,Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?
6. Wa hao wanaozitumainia mali zao,Na kujisifia wingi wa utajiri wao;
7. Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake,Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,
8. (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama,Wala hana budi kuiacha hata milele;)
9. ili aishi sikuzote asilione kaburi.