2. Watu wakuu na watu wadogo wote pia,Tajiri na maskini wote pamoja.
3. Kinywa changu kitanena hekima,Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara.
4. Nitatega sikio langu nisikie mithali,Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi
5. Kwa nini niogope siku za uovu,Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?
6. Wa hao wanaozitumainia mali zao,Na kujisifia wingi wa utajiri wao;