15. Bali Mungu atanikomboa nafsi yangu,Atanitoa mkononi mwa kuzimu, maana atanikaribisha.
16. Usiogope mtu atakapopata utajiri,Na fahari ya nyumba yake itakapozidi.
17. Maana atakapokufa hatachukua cho chote;Utukufu wake hautashuka ukimfuata.
18. Ajapojibariki nafsi yake alipokuwa hai,Na watu watakusifu ukijitendea mema,
19. Atakwenda kwenye kizazi cha baba zakeHawataona nuru hata milele.