Zab. 49:1-9 Swahili Union Version (SUV)

1. Sikieni haya, enyi mataifa yote;Sikilizeni, ninyi nyote mnaokaa duniani.

2. Watu wakuu na watu wadogo wote pia,Tajiri na maskini wote pamoja.

3. Kinywa changu kitanena hekima,Na fikira za moyo wangu zitakuwa za busara.

4. Nitatega sikio langu nisikie mithali,Na kufumbua fumbo langu kwa kinubi

5. Kwa nini niogope siku za uovu,Ubaya ukinizunguka miguuni pangu?

6. Wa hao wanaozitumainia mali zao,Na kujisifia wingi wa utajiri wao;

7. Hakuna mtu awezaye kumkomboa ndugu yake,Wala kumpa Mungu fidia kwa ajili yake,

8. (Maana fidia ya nafsi zao ina gharama,Wala hana budi kuiacha hata milele;)

9. ili aishi sikuzote asilione kaburi.

Zab. 49