4. Atatuchagulia urithi wetu,Fahari ya Yakobo ambaye alimpenda.
5. Mungu amepaa kwa kelele za shangwe,BWANA kwa sauti ya baragumu.
6. Mwimbieni Mungu, naam, imbeni;Mwimbieni mfalme wetu, naam, imbeni.
7. Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,Imbeni kwa akili.
8. Mungu awamiliki mataifa,Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu.