6. Mataifa yalighadhibika, falme zikataharuki;Alitoa sauti yake, nchi ikayeyuka.
7. BWANA wa majeshi yu pamoja nasi,Mungu wa Yakobo ni ngome yetu.
8. Njoni myatazame matendo ya BWANA,Jinsi alivyofanya ukiwa katika nchi.
9. Avikomesha vita hata mwisho wa dunia;Avunja uta, akata mkuki, achoma moto magari.
10. Acheni, mjue ya kuwa Mimi ni Mungu,Nitakuzwa katika mataifa, nitakuzwa katika nchi.