1. Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu,Msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso.
2. Kwa hiyo hatutaogopa ijapobadilika nchi,Ijapotetemeka milima moyoni mwa bahari.
3. Maji yake yajapovuma na kuumuka,Ijapopepesuka milima kwa kiburi chake.
4. Kuna mto, vijito vyake vyaufurahisha mji wa Mungu,Patakatifu pa maskani zake Aliye juu.