Zab. 45:6-9 Swahili Union Version (SUV)

6. Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele,Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.

7. Umeipenda haki;Umeichukia dhuluma.Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta,Mafuta ya furaha kuliko wenzako.

8. Mavazi yako yote hunukia manemaneNa udi na mdalasini.Katika majumba ya pembeVinubi vimekufurahisha.

9. Binti za wafalme wamoMiongoni mwa akina bibi wako wastahiki.Mkono wako wa kuume amesimama malkiaAmevaa dhahabu ya Ofiri.

Zab. 45