4. Katika fahari yako usitawi uendeleeKwa ajili ya kweli na upole na hakiNa mkono wako wa kuumeUtakufundisha mambo ya kutisha.
5. Mishale yako ni mikali, watu huanguka chini yako;Imo mioyoni mwa adui za mfalme.
6. Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele,Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
7. Umeipenda haki;Umeichukia dhuluma.Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekupaka mafuta,Mafuta ya furaha kuliko wenzako.