7. Wote wanaonichukia wananinong’ona,Wananiwazia mabaya.
8. Neno la kisirani limemgandama,Na iwapo amelala hatasimama tena.
9. Msiri wangu tena niliyemtumaini,Aliyekula chakula changu,Ameniinulia kisigino chake.
10. Lakini Wewe, BWANA, unifadhili,Uniinue nipate kuwalipa.
11. Kwa neno hili nimejua ya kuwa wapendezwa nami,Kwa kuwa adui yangu hasimangi kwa kunishinda.
12. Nami katika ukamilifu wangu umenitegemeza,Umeniweka mbele za uso wako milele.