1. Nalisema, Nitazitunza njia zanguNisije nikakosa kwa ulimi wangu;Nitajitia lijamu kinywani,Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu.
2. Nalikuwa sisemi, nalinyamaa kimya,Sina faraja, maumivu yangu yakazidi.
3. Moyo wangu ukawa moto ndani yangu,Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka;Nalisema kwa ulimi wangu,
4. BWANA, unijulishe mwisho wangu,Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani;Nijue jinsi nilivyo dhaifu.
5. Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri;Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako.Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.
6. Binadamu huenda tu huko na huko kama kivuli;Hufanya ghasia tu kwa ajili ya ubatili;Huweka akiba wala hajui ni nani atakayeichukua.
7. Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana?Matumaini yangu ni kwako.
8. Uniokoe na maasi yangu yote,Usinifanye laumu ya mpumbavu.
9. Nimenyamaza, sitafumbua kinywa changu,Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.