Zab. 39:1-7 Swahili Union Version (SUV)

1. Nalisema, Nitazitunza njia zanguNisije nikakosa kwa ulimi wangu;Nitajitia lijamu kinywani,Maadamu mtu mbaya yupo mbele yangu.

2. Nalikuwa sisemi, nalinyamaa kimya,Sina faraja, maumivu yangu yakazidi.

3. Moyo wangu ukawa moto ndani yangu,Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka;Nalisema kwa ulimi wangu,

4. BWANA, unijulishe mwisho wangu,Na kiasi cha siku zangu ni kiasi gani;Nijue jinsi nilivyo dhaifu.

5. Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri;Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako.Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.

6. Binadamu huenda tu huko na huko kama kivuli;Hufanya ghasia tu kwa ajili ya ubatili;Huweka akiba wala hajui ni nani atakayeichukua.

7. Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana?Matumaini yangu ni kwako.

Zab. 39