Zab. 38:13-21 Swahili Union Version (SUV)

13. Lakini kama kiziwi sisikii,Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake.

14. Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia,Ambaye hamna hoja kinywani mwake.

15. Kwa kuwa nakungoja Wewe, BWANA,Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu.

16. Maana nalisema, Wasije wakanifurahia;Mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu.

17. Kwa maana mimi ni karibu na kusita,Na maumivu yangu yako mbele yangu daima.

18. Kwa maana nitaungama uovu wangu,Na kusikitika kwa dhambi zangu.

19. Lakini adui zangu ni wazima wenye nguvu,Nao wanaonichukia bure wamekuwa wengi.

20. Naam, wakilipa mabaya kwa mema,Huwa adui zangu kwa kuwa nalifuata lililo jema.

21. Wewe, BWANA, usiniache,Mungu wangu, usijitenge nami.

Zab. 38