Zab. 38:10-16 Swahili Union Version (SUV)

10. Moyo wangu unapwita-pwita,Nguvu zangu zimeniacha;Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.

11. Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu;Naam, karibu zangu wamesimama mbali.

12. Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego;Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya;Na kufikiri hila mchana kutwa.

13. Lakini kama kiziwi sisikii,Nami ni kama bubu asiyefumbua kinywa chake.

14. Naam, nimekuwa kama mtu asiyesikia,Ambaye hamna hoja kinywani mwake.

15. Kwa kuwa nakungoja Wewe, BWANA,Wewe utajibu, Ee Bwana, Mungu wangu.

16. Maana nalisema, Wasije wakanifurahia;Mguu wangu ukiteleza wajitukuza juu yangu.

Zab. 38