Zab. 38:1-12 Swahili Union Version (SUV)

1. Ee BWANA, usinilaumu katika ghadhabu yako,Wala usiniadhibu kwa ukali wa hasira yako.

2. Kwa maana mishale yako imenichoma,Na mkono wako umenipata.

3. Hamna uzima katika mwili wanguKwa sababu ya ghadhabu yako.Wala hamna amani mifupani mwanguKwa sababu ya hatia zangu.

4. Maana dhambi zangu zimenifunikiza kichwa,Kama mzigo mzito zimenilemea mno.

5. Jeraha zangu zinanuka, zimeoza,Kwa sababu ya upumbavu wangu.

6. Nimepindika na kuinama sana,Mchana kutwa nimekwenda nikihuzunika.

7. Maana viuno vyangu vimejaa homa,Wala hamna uzima katika mwili wangu.

8. Nimedhoofika na kuchubuka sana,Nimeugua kwa fadhaa ya moyo wangu.

9. Bwana, haja zangu zote ziko mbele zako,Kuugua kwangu hakukusitirika kwako.

10. Moyo wangu unapwita-pwita,Nguvu zangu zimeniacha;Nuru ya macho yangu nayo imeniondoka.

11. Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu;Naam, karibu zangu wamesimama mbali.

12. Nao wanaoutafuta uhai wangu hutega mitego;Nao wanaotaka kunidhuru hunena mabaya;Na kufikiri hila mchana kutwa.

Zab. 38