Zab. 37:32-35 Swahili Union Version (SUV)

32. Mtu asiye haki humvizia mwenye haki,Na kutafuta jinsi ya kumfisha.

33. BWANA hatamwacha mkononi mwake,Wala hatamlaumu atakapohukumiwa.

34. Wewe umngoje BWANA,Uishike njia yake,Naye atakutukuza uirithi nchi,Wasio haki watakapoharibiwa utawaona.

35. Nimemwona mtu asiye haki mkali sana,Akijieneza kama mwerezi wa Lebanoni.

Zab. 37