16. Kidogo alicho nacho mwenye haki ni boraKuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.
17. Maana mikono ya wasio haki itavunjika,Bali BWANA huwategemeza wenye haki.
18. BWANA anazijua siku za wakamilifu,Na urithi wao utakuwa wa milele.
19. Hawataaibika wakati wa ubaya,Na siku za njaa watashiba.
20. Bali wasio haki watapotea,Nao wamchukiao BWANA watatoweka,Kama uzuri wa mashamba,Kama moshi watatoweka.
21. Asiye haki hukopa wala halipi,Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.
22. Maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi,Nao waliolaaniwa na yeye wataharibiwa.
23. Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA,Naye aipenda njia yake.
24. Ajapojikwaa hataanguka chini,BWANA humshika mkono na kumtegemeza.
25. Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee,Lakini sijamwona mwenye haki ameachwaWala mzao wake akiomba chakula.
26. Mchana kutwa hufadhili na kukopesha,Na mzao wake hubarikiwa.
27. Jiepue na uovu, utende mema,Na kukaa hata milele.
28. Kwa kuwa BWANA hupenda haki,Wala hawaachi watauwa wake.Wao hulindwa milele,Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa.
29. Wenye haki watairithi nchi,Nao watakaa humo milele.