10. Maana bado kitambo kidogo asiye haki hatakuwapo,Utapaangalia mahali pake wala hatakuwapo.
11. Bali wenye upole watairithi nchi,Watajifurahisha kwa wingi wa amani.
12. Asiye haki hunuia mabaya juu ya mwenye haki,Na kumsagia meno yake.
13. BWANA atamcheka,Maana ameona kwamba siku yake inakuja.
14. Wasio haki wamefuta upanga na kupinda uta,Wamwangushe chini maskini na mhitaji,Na kuwaua wenye mwenendo wa unyofu.
15. Upanga wao utaingia mioyoni mwao wenyewe,Na nyuta zao zitavunjika.
16. Kidogo alicho nacho mwenye haki ni boraKuliko wingi wa mali wa wasio haki wengi.
17. Maana mikono ya wasio haki itavunjika,Bali BWANA huwategemeza wenye haki.
18. BWANA anazijua siku za wakamilifu,Na urithi wao utakuwa wa milele.
19. Hawataaibika wakati wa ubaya,Na siku za njaa watashiba.
20. Bali wasio haki watapotea,Nao wamchukiao BWANA watatoweka,Kama uzuri wa mashamba,Kama moshi watatoweka.
21. Asiye haki hukopa wala halipi,Bali mwenye haki hufadhili, hukirimu.
22. Maana waliobarikiwa na yeye watairithi nchi,Nao waliolaaniwa na yeye wataharibiwa.
23. Hatua za mtu zaimarishwa na BWANA,Naye aipenda njia yake.
24. Ajapojikwaa hataanguka chini,BWANA humshika mkono na kumtegemeza.
25. Nalikuwa kijana nami sasa ni mzee,Lakini sijamwona mwenye haki ameachwaWala mzao wake akiomba chakula.
26. Mchana kutwa hufadhili na kukopesha,Na mzao wake hubarikiwa.
27. Jiepue na uovu, utende mema,Na kukaa hata milele.
28. Kwa kuwa BWANA hupenda haki,Wala hawaachi watauwa wake.Wao hulindwa milele,Bali mzao wa wasio haki ataharibiwa.
29. Wenye haki watairithi nchi,Nao watakaa humo milele.