1. Usikasirike kwa sababu ya watenda mabaya,Usiwahusudu wafanyao ubatili.
2. Maana kama majani watakatika mara,Kama miche mibichi watanyauka.
3. Umtumaini BWANA ukatende mema,Ukae katika nchi, upendezwe na uaminifu.
4. Nawe utajifurahisha kwa BWANA,Naye atakupa haja za moyo wako.
5. Umkabidhi BWANA njia yako,Pia umtumaini, naye atafanya.
6. Ataitokeza haki yako kama nuru,Na hukumu yako kama adhuhuri.