Zab. 34:13-17 Swahili Union Version (SUV)

13. Uuzuie ulimi wako na mabaya,Na midomo yako na kusema hila.

14. Uache mabaya ukatende mema,Utafute amani ukaifuatie.

15. Macho ya BWANA huwaelekea wenye haki,Na masikio yake hukielekea kilio chao.

16. Uso wa BWANA ni juu ya watenda mabaya,Aliondoe kumbukumbu lao duniani.

17. Walilia, naye BWANA akasikia,Akawaponya na taabu zao zote.

Zab. 34