1. Nitamhimidi BWANA kila wakati,Sifa zake zi kinywani mwangu daima.
2. Katika BWANA nafsi yangu itajisifu,Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
3. Mtukuzeni BWANA pamoja nami,Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
4. Nalimtafuta BWANA akanijibu,Akaniponya na hofu zangu zote.
5. Wakamwelekea macho wakatiwa nuru,Wala nyuso zao hazitaona haya.