5. Huzipenda haki na hukumu,Nchi imejaa fadhili za BWANA.
6. Kwa neno la BWANA mbingu zilifanyika,Na jeshi lake lote kwa pumzi ya kinywa chake.
7. Hukusanya maji ya bahari chungu chungu,Huviweka vilindi katika ghala.
8. Nchi yote na imwogope BWANA,Wote wakaao duniani na wamche.
9. Maana Yeye alisema, ikawa;Na Yeye aliamuru, ikasimama.
10. BWANA huyabatilisha mashauri ya mataifa,Huyatangua makusudi ya watu.
11. Shauri la BWANA lasimama milele,Makusudi ya moyo wake vizazi na vizazi.
12. Heri taifa ambalo BWANA ni Mungu wao,Watu aliowachagua kuwa urithi wake.
13. Toka mbinguni BWANA huchungulia,Huwatazama wanadamu wote pia.
14. Toka mahali pake aketipoHuwaangalia wote wakaao duniani.
15. yeye aiumbaye mioyo yao woteHuzifikiri kazi zao zote.
16. Hapana mfalme aokokaye kwa wingi wa uwezo,Wala shujaa haokoki kwa wingi wa nguvu.
17. Farasi hafai kitu kwa wokovu,Wala hamponyi mtu kwa wingi wa nguvu zake.