18. Tazama, jicho la BWANA li kwao wamchao,Wazingojeao fadhili zake.
19. Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,Na kuwahuisha wakati wa njaa.
20. Nafsi zetu zinamngoja BWANA;Yeye ndiye msaada wetu na ngao yetu.
21. Maana mioyo yetu itamfurahia,Kwa kuwa tumelitumainia jina lake takatifu.