Zab. 33:1-4 Swahili Union Version (SUV)

1. Mpigieni BWANA vigelegele, enyi wenye haki,Kusifu kunawapasa wanyofu wa moyo.

2. Mshukuruni BWANA kwa kinubi,Kwa kinanda cha nyuzi kumi mwimbieni sifa.

3. Mwimbieni wimbo mpya,Pigeni kwa ustadi kwa sauti ya shangwe.

4. Kwa kuwa neno la BWANA lina adili,Na kazi yake yote huitenda kwa uaminifu.

Zab. 33