8. Wala hukunitia mikononi mwa adui;Miguu yangu umeisimamisha panapo nafasi.
9. Ee BWANA, unifadhili, maana ni katika dhiki,Jicho langu limenyauka kwa masumbufu,Naam, mwili wangu na nafsi yangu.
10. Maana maisha yangu yamekoma kwa huzuni,Na miaka yangu kwa kuugua.Nguvu zangu zinatetemeka kwa uovu wangu,Na mifupa yangu imekauka.
11. Kwa sababu ya watesi wangu nimekuwa laumu,Naam, hasa kwa jirani zangu;Na kitu cha kutisha kwa rafiki zangu;Walioniona njiani walinikimbia.
12. Nimesahauliwa kama mfu asiyekumbukwa;Nimekuwa kama chombo kilichovunjika.
13. Maana nimesikia masingizio ya wengi;Hofu ziko pande zote.Waliposhauriana juu yangu,Walifanya hila wauondoe uhai wangu.
14. Lakini mimi nakutumaini Wewe, BWANA,Nimesema, Wewe ndiwe Mungu wangu.
15. Nyakati zangu zimo mikononi mwako;Uniponye na adui zangu, nao wanaonifuatia.
16. Umwangaze mtumishi wakoKwa nuru ya uso wako;Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
17. Ee BWANA, nisiaibishwe, maana nimekuita;Waaibishwe wasio haki, wanyamaze kuzimuni.