1. Nimekukimbilia Wewe, BWANA,Nisiaibike milele.Kwa haki yako uniponye,
2. Unitegee sikio lako, uniokoe hima.Uwe kwangu mwamba wa nguvu,Nyumba yenye maboma ya kuniokoa.
3. Ndiwe genge langu na ngome yangu;Kwa ajili ya jina lako uniongoze, unichunge.
4. Utanitoa katika wavu walionitegea kwa siri,Maana Wewe ndiwe ngome yangu.
5. Mikononi mwako naiweka roho yangu;Umenikomboa, Ee BWANA, Mungu wa kweli.
6. Nawachukia wao washikao yasiyofaa yenye uongo;Bali mimi namtumaini BWANA.