6. Nitanawa mikono yangu kwa kutokuwa na hatia,Na kuizunguka madhabahu yako, Ee BWANA
7. Ili niitangaze sauti ya kushukuru,Na kuzisimulia kazi zako za ajabu.
8. BWANA, nimependa makao ya nyumba yako,Na mahali pa maskani ya utukufu wako.
9. Usiiondoe nafsi yangu pamoja na wakosaji,Wala uhai wangu pamoja na watu wa damu.
10. Mikononi mwao mna madhara,Na mkono wao wa kuume umejaa rushwa.