Zab. 22:2-6 Swahili Union Version (SUV)

2. Ee Mungu wangu, nalia mchana lakini hujibuNa wakati wa usiku lakini sipati raha.

3. Na Wewe U Mtakatifu,Uketiye juu ya sifa za Israeli.

4. Baba zetu walikutumaini Wewe,Walitumaini, na Wewe ukawaokoa.

5. Walikulilia Wewe wakaokoka,Walikutumaini wasiaibike.

6. Lakini mimi ni mdudu wala si mtu,Laumu ya wanadamu na mzaha wa watu.

Zab. 22