5. Na tuushangilie wokovu wako,Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu.BWANA akutimizie matakwa yako yote.
6. Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake;Atamjibu toka mbingu zake takatifu,Kwa matendo makuu ya wokovuYa mkono wake wa kuume.
7. Hawa wanataja magari na hawa farasi,Bali sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.
8. Wao wameinama na kuanguka,Bali sisi tumeinuka na kusimama.