Zab. 2:6-11 Swahili Union Version (SUV)

6. Nami nimemweka mfalme wanguJuu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

7. Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia,Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

8. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,Na miisho ya dunia kuwa milki yako.

9. Utawaponda kwa fimbo ya chuma,Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi.

10. Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili,Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe.

11. Mtumikieni BWANA kwa kicho,Shangilieni kwa kutetemeka.

Zab. 2