Zab. 2:1-8 Swahili Union Version (SUV)

1. Mbona mataifa wanafanya ghasia,Na makabila wanatafakari ubatili?

2. Wafalme wa dunia wanajipanga,Na wakuu wanafanya shauri pamoja,Juu ya BWANA,Na juu ya masihi wake,

3. Na tuvipasue vifungo vyao,Na kuzitupia mbali nasi kamba zao.

4. Yeye aketiye mbinguni anacheka,Bwana anawafanyia dhihaka.

5. Ndipo atakaposema nao kwa hasira yake,Na kuwafadhaisha kwa ghadhabu yake.

6. Nami nimemweka mfalme wanguJuu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.

7. Nitaihubiri amri; BWANA aliniambia,Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.

8. Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,Na miisho ya dunia kuwa milki yako.

Zab. 2