7. Dhihirisha fadhili zako za ajabuWewe uwaokoaye wanaokukimbilia;Kwa mkono wako wa kuumeUwaokoe nao wanaowaondokea.
8. Unilinde kama mboni ya jicho,Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
9. Wasinione wasio haki wanaonionea,Adui za roho yangu wanaonizunguka.
10. Wameukaza moyo wako,Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.
11. Sasa wametuzunguka hatua zetu,Na kuyakaza macho yao watuangushe chini.